Tuesday, 20 October 2015

Chopa ya Lusinde yapata hitilafu, Mwenyewe aapa kutoipanda

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ameapa kutotumia tena usafiri wa anga katika kampeni, baada ya helikopta aliyokuwa anatumia kupata hitilafu na kushindwa kuruka katika Kijiji cha Idifu wilayani hapa, juzi.

Lusinde maarufu kwa jina la Kibajaji alithibitisha kuwa helikopta hiyo ilishindwa kuruka baada ya rubani kubaini ilikuwa na hitilafu, na ilikuwa imetua katika eneo la kichaka kijijini hapo.


No comments: