Saturday, 10 October 2015

Kayumba Juma Ajinyakulia Mil,50 za Fainali za Bongo Star Search (Season 8, 2015)

Mshindi BSS 2015,Kayumba Juma.
Kijana mdogo{16yrs}akiwakilisha jiji la Dar es salaam kwenye Shindano la kusaka Vipaji BONGO{BSS} jana alifanikiwa kuanza kutimiza moja ya NDOTO zake maishani baada ya kufanikiwa kushinda Shilingi Mil 50 Za Shindano hilo Maarufu la kusaka Vipaji katika Sanaa ya Muziki nchini TANZANIA.
Tumekuletea Mtiririko Mzima wa Shindano hilo uliopelekea kijana Kayumba Juma kutawazwa Mshindi wa Shindano hilo,Fuatilia yaliyojiri hapo chini.......
 Ikiwa ni fainali ya mashindano haya. Washiriki walioingia FAINALI wapo 6, na anahitajika mshindi mmoja atakayeibuka na kitita cha shilingi milioni 50 Usiku huu.
==============

Mchuano umeanza, kwa ushindani mkali sana .

Wapo washiriki sita, wanahitajika watano waweze kuingia top 5.

Kila mshiriki ataimba wimbo mmoja ili mchujo upite wabakie watano.
=================

- Waimbaji wote sita mpaka sasa wameshaimba nyimbo mojamoja. Majaji wanachuja majina sita yapatikane matano.
- Kampuni ya Huawei kupitia wawakilishi wake wanagawa zawadi ya simu kwa washiriki wote sita.

WALIOINGIA TOP 5:
- Wafuatao wamechaguliwa kuingia 5 bora;

1.Kayumba Juma
2.Angel Marry Kato
3.Nasib Fenabo
4.Frida Amani
5.Kevin Gerson

- Mshiriki aliyeshindwa kufuzu ni Jackline, anatoka katika mashindano.

==================


MC wa BSS, Ceasar Daniel azua gumzo!

Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mtangazaji muongozaji wa Bongo Star Search Caesar Daniel amekuja na Msemo wa #HapaKaziTu.

Hali imebadilika ghafla ukumbi ukalipuka mabadiliko, huku wahdhuriaji wakionesha vidole viwili kuashiria alama ya chama cha siasa na wengine wakizungusha mikono kuonesha Mabadilikoooooo..

Kazi kweli kweli!

WALIOINGIA TOP 3:
- Wafuatao wamechaguliwa kuingia kwenye 3 bora;

1. Nasib Fenabo
2. Frida Amani
3. Kayumba Juma

- Walioshindwa kuingia kwenye awamu hii ni Kevin Gerson na Angel Marry Kato.
===============

WALIOINGIA TOP 2:
- Waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia kwenye 2 bora ni;

1. Kayumba Juma
2. Nasib Fenabo..

- Burudani zinaendelea kabla ya kuingia kwenye awamu ya mwisho kumpata Bongo Super Star - 2015

- Jukwaani anapanda Christian Bella na Malaika Band.

- Si mchezo! Show anayoifanya Bella inamfanya kutuzwa pesa nyingi mno.. Amekonga nyoyo za waliohudhuria hapa!
===========



- Na sasa ni wakati wa msanii Runtown kutoka Nigeria kutumbuiza. Anapanda na dancers wake jukwaani.
Kumbuka
Huyu ndiye msanii wa mwisho 'kupafomu' kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha mwisho kumpata mshindi wa BSS 2015.
===========================

Naam, na sasa ule muda uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu umewadia!

- Chief Judge, Madam Rittah amepanda jukwaani kuungana na washereheshaji Caesar Daniel na Penny kumtangaza Mshindi. Je, ni Kayumba au Fenabo?

Madam Rittah

Kwa kweli najisikia faraja sana kufikia hatua hii. Napenda kutoa shukrani kwa tulioshirikiana kulifanikisha hili (anataja timu ya BSS, Majaji wenza, Wadhamini na wadau mbalimbali).

- Na Mshindi wa BSS 2015 (Season 8) ni.....

Kayumba Juma-Winner-"BONGO STAR SEARCH 2015".

No comments: