Wednesday, 21 October 2015

Madereva wa Malori wamefunga Barabara ya Morogoro, baada ya mwenzao kupigwa risasi na mwajiri wake.

Habari za asubuh hii zinasema Madereva wa Malori wameamua kuacha Magari yao njiani, ni baada ya mwenzao kukwatuliwa Risas Bandarini jana, Magari hayatembei kabisa toka Kibaha kuja Ubungo.

TAARIFA:-
Quote By Dotto Mnzava View Post
Kuna shuhuda ambaye yupo eneo la tukio, amesema kuna dereva wa lori ambaye ameiba mafuta kwenye gari kiasi cha lita 300 ambayo ni mali ya kampuni anayofanyia kazi (haikutambulika mara moja) kisha akampigia simu bosi wake kuwa gari limepata ajali na linawaka moto.

Baada ya hapo bosi wake alipomwambia dereva kuwa asubiri hapo hapo ili aje washughulikie tatizo lakini bosi wake alivyofika eneo la tukio akakuta kuwa amedanganywa kwamaana kwamba maelezo ya marafiki zake na marehemu yanaeleza kuwa dereva alikuwa anataka kumwambia mwajiri wake kuwa baada ya ajali wananchi wamechota mafuta na pia alipanga baada ya muda alipige kiberiti gari.

Bosi wake anapatikana hapa Dar es Salaam na hivyo bosi wake alichukua pikipiki ili kufika katika eneo la tukio. Alivyokuja na kukuta hali ni tofauti aliamua kumpiga risasi ya kichwa dereva na kuondoka zake.

"Mgomo wa madereva umeanzia Kibaha kwa Mfipa japokuwa watu wengine hapa nilipo wanasema sakata hili limeanzia Mbagala"
 
Quote By Milindi View Post
Wakati Bonge anaripoti kwenye PB.Alihojiwa katibu wa madereva na kusema kuwa Dereva aliyeuawa alipata shot ya mafuta wakati anarudisha tank yard ndio bosi wake akampiga risasi ya kichwa.Kwa jinsi nilivyosikia redioni itakuwa vita kubwa sana lets wait.Je Lita 300 ndio ina thamani kubwa ya uhai wa binadamu!!??.Madreva wa kampuni hiyo wameripoti mara nyingi kutishiwa kuuawa na wameripoti mara nyingi polisi chang'ombe lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.{source-Bonge PB}
 
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura, ameithibitishia JamiiForums kupokea taarifa za mgomo huo na kwamba anafuatilia ili kujua kama taarifa hizo zina ukweli kiasi gani. Atatoa taarifa kamili baada ya muda.
 
Chanzo-JamiiForum 
 

No comments: