Tuesday, 27 October 2015

MAWAZIRI WA SERIKALI ILIYOPITA WALIOKWISHA PIGWA CHINI MPAKA SASA{UCHAGUZI MKUU 2015}

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira,
Baadhi ya Mawaziri na vigogo kadhaa  wameanguka na kupoteza viti vyao vya ubunge katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi.
Miongoni mwa walioanguka hadi jana wakati matokeo ya uchaguzi huo yakiendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, ambaye melipoteza Jimbo la Bunda, mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela, amekwama kutetea jimbo lake la Same Mashariki, mkoani Kilimanjaro.
Mwingine aliyepoteza ubunge ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwezeshaji na Uwekezaji), Christopher Chiza, katika Jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwezeshaji na Uwekezaji), Christopher Chiza

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri, ameanguka na kulipoteza jimbo la Siha, mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri

DK. Kebwe Stephen Kebwe, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ameangushwa katika Jimbo la Serengeti, mkoani Mara, baada ya kupata kura 39,232 dhidi ya 40,059 za mpinzani wake, Marwa Ryoba wa Chadema.

DK. Kebwe Stephen Kebwe, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mbunge wa Same Magharibi, Dk. David Mathayo David (CCM), ameanguka na kushindwa kutetea kiti chake, baada ya kuangushwa na mgombea wa Chadema, Christopher Mbajo, ambaye alipata kura 21,418 dhidi ya kura 15, 347 dhidi ya Dk. Mathayo.

No comments: