Polisi
wanne waliokuwa doria wakati wa uchaguzi juzi usiku, walijikuta
wakionja machungu ya maji ya kuwasha, baada ya kumwagiwa na wenzao
wakati wakijaribu kuwatawanya wafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) waliokuwa wakisherehekea matokeo ya udiwani.
Kufuatia tukio hilo katika Kata ya Makumbusho, Dar es Salaam, askari hao walijikuta mikononi mwa raia wakipatiwa msaada wa huduma ya kwanza kutokana na gari lao kumwagiwa maji ya kuwasha, kufuatia gari lililokuwa mbele yao kufyatuka pampu na kuanza kurusha maji hayo.
Tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Mwananyamala A, karibu na nyumba za makazi ya watu, wakati magari matano ya askari yakiwa nyuma ya gari lenye maji ya kuwasha, wakijaribu kutuliza ghasia za wananchi waliokuwa wakiandamana kushangilia ushindi wa diwani aliyeshinda, Harub Ally.
Chanzo:-Times Fm

No comments:
Post a Comment