Taarifa za Ajali hii zimethibitishwa na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala Bw,Jerry Slaa ambaye pia amempoteza baba yake mzazi kwenye ajali hiyo.
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa toka kwa Kikosi cha uokoaji ambao wamefika eneo la tukio na kukuta tayari watu wote waliokuwemo kwenye helikopta hiyo iliyopata ajali akiwemo Rubani ambaye pia ni Baba yangu Capt William Slaa wamekwisha Fariki dunia" amesema Jerry Slaa
Ajali hiyo imetokea jana usiku ambapo Capt William Slaa na Mh,Deo Filikunjombe wakiwa na Abiria wengine ndani ya Helikopta No-5Y-DKK ambapo walikuwa wakielekea Ludewa{Mbeya}
wakitokea jijini Dar es salaam.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU PEMA PEPONI..
No comments:
Post a Comment