Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete ni miongni mwa viongozi wapenda michezo waliowahi kuiongoza Tanzania.
Rais Kikwete
ambaye kuanzia mwaka 2006 alianza kurudisha morali kwa wapenzi na
mashabiki wa soka ili wazidi kuipenda timu yao ya taifa, amebakiza siku
kadhaa kabla ya kuondoka madarakani.
Miongoni mwa mambo aliyoyafanya Rais Kikwete ni pamoja na kukubali kuwalipa makocha wa timu za taifa, hivyo usiku wa October 12 chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) kiliandaa Tuzo ya heshima kwa ajili ya Rais Kikwete hii ikiwa ni pamoja na kumuaga. Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, lakini alikuwa na haya ya kusema kuhusu michezo Tanzania.
“Kwenye michezo tusipofanya vizuri
huwa na sononeka sana, ndio maana wakati naingia madarakani mwaka 2005
nilisema mchango nitakao utoa ni kuajiri makocha. Lakini mimi nasema
michezo nchini tatizo kubwa ni uongozi, kwani watu wengi wanapenda
uongozi kwa heshima ya cheo, sasa mimi mchango wangu wa mwisho nitakao
toa katika michezo ni kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya soka
nchini, tarehe 17 tunakizindua pale kidongo chekundu”
Hizi ni dakika tatu za hotuba ya Rais Kikwete msikilize Hapo chini....


No comments:
Post a Comment