![]() |
Yang Feng Glan“Ivory Queen” |
Mwanamke wa China anayedaiwa kuongoza genge kubwa zaidi la usafirishaji pembe za ndovu barani Afrika amekamatwa nchini.
Akipewa
jina la utani “Ivory Queen”, Yang Feng Glan anadaiwa kusafirisha pembe
za ndovu 706 kutoka nchini kwenda Mashariki ya mbali.
Glan,
66, anadaiwa kuwa na ukaribu na majangili wa Afrika Mashariki na
walanguzi wa China. Anadaiwa pia kuyasaidia kifedha makundi ya majangili
zinazoyasaidia kununua silaha na magari na pia kutoa rushwa ili kufanya
kazi bila vikwazo.
Mama
huyo alifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na
anashtakiwa kwa kusafirisha pembe za ndovu zenye thamani ya paundi
milioni 1.62 katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2014 ingawa wapelelezi
wanaamini amekuwa akifanya kazi hiyo tangu miaka 1980.
Alifikishwa
mahakamani akiwa na wanaume wawili raia wa Tanzania ambao wamekuwa
wasaidizi wake wakuu. Anaendelea kushikiliwa na polisi.
Kukamatwa kwa mama huyo kumekuja baada ya kuwepo upelelezi wa mwaka mzima na kikosi cha kukabiliana na ujangili.
Chanzo: Bongo 5
No comments:
Post a Comment