![]() |
| Samir Nasri |
Samir Nasri ambaye amenukuliwa akisema hawezi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa hata kama baba yake mzazi angechaguliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Samir Nasri ambaye amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya wakubwa kuanzia mwaka 2007 hadi 2013, alitangaza kustaafu soka kuichezea Ufaransa August 2014 baada ya kocha wa Ufaransa Didier Deschamps kumuacha katika kikosi cha Ufaransa kilichocheza Kombe la Dunia 2014.
“Hata
kama baba yangu akichaguliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa
siwezi kurudi kuichezea, nimeangaika kucheza vizuri ili
nichachaguliwe timu ya taifa lakini nikakosa Kombe la Dunia 2014, Mpango
wangu ulikuwa ni kustaafu timu ya taifa toka 2012 ila baba yangu
alinishauri nicheze kombe la Dunia 2014 kwa sababu nilikuwa na kiwango
kizuri”>>> Nasri
Samir Nasri amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa
michezo 41 na kufunga magoli 5 katika kipindi cha mwaka 2007-2013,
ameoneshwa kuudhunishwa na tukio la kuachwa kwake katika kikosi
kilichocheza Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Nasri amejibu hayo baada ya kuulizwa kama anaweza kurejea kuichezea Ufaransa. Sababu za kuachwa kwa Samir Nasri katika Kombe la Dunia 2014 zinatajwa kuwa sio za kushuka kiwango ila ni tofauti zake Didier Deschamps.
![]() |
| Didier Deschamps. |




No comments:
Post a Comment