Mimi na Mh Duni tumewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
— Edward Lowassa (@edwardlowassatz) October 29, 2015
Ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD LOWASSA kuwa mshindi nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania
— Edward Lowassa (@edwardlowassatz) October 29, 2015
Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua,sisi tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani.
— Edward Lowassa (@edwardlowassatz) October 29, 2015
Tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko na viongozi mnao wahitaji. Nitaendelea kudai haki kwa nguvu zote
— Edward Lowassa (@edwardlowassatz) October 29, 2015
unashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita. 1/2
— Edward Lowassa (@edwardlowassatz) October 29, 2015
Kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, watanzania hatutakubali hali hiyo.2/2
— Edward Lowassa (@edwardlowassatz) October 29, 2015
Takwimu zetu zilionesha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.
— Edward Lowassa (@edwardlowassatz) October 29, 2015

No comments:
Post a Comment