Tuesday, 17 November 2015

ALIKIBA AFUNGUKA NJAMA ZILIZOPELEKEA KUKOSA TUZO ZA AFRIMA-NIGERIA.

Staa wa Bongo Fleva Ali Kiba kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika kuwa pamoja na kupigiwa kura sana na mashabiki wake lakini amegundua baada ya kufuatilia kuwa kuna mambo yanayoendelea ya watu wanaodiriki hata kupoteza pesa zao kwa ajili yake.

‘’Asanteni Sana Najua Mmepiga Kura Sana Lakini Nilikuja Kugundua Baada Yakufatilia Kuwa Kuna Mambo Yanaendelea Ya Watu Wana Diriki Hata Kupoteza Pesa Zao Kwaajili Yangu Ila Nawaomba Fans Msinielewe Vibaya I will Always Be There For You #HapaKaziTu #KingKiba’’ 


Ali Kiba ameshindwa kunyakuwa tuzo za AFRIMMA za nchini Nigeria zilizofanyika jana huku mpinzani wake Diamond akinyakua tuzo tatu.

No comments: