Mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es Salaam imemkuta na hatia
aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la ndege la taifa ATCL Bw David Mattaka
na wenzake wawili baada ya mashahidi 13 kutoa ushahidi wao mahakamni
hapo.
Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo Emmilius Mchauru amesema
mahakama imejiridhisha bila shaka baada ya upande wa mashitaka
kuwasilisha mashahidi 13 kuhusu tuhuma zinazomkabili kigogo huyo wa
zamani wa ATCL za matumizi mabaya ya ofisi kwa kutangaza zabuni ya
ununuzi wa magari yaliyochakaa 26 na kuisababishia hasara serikali ya
mabilioni ya shilingi.
Washitakiwa wote watatu wakiongozwa na mawakili wao walikubali
kutoa ushahidi wao kwa kula kiapo ambapo mashahidi wa washitakiwa hao
wanatarajiwa kuanza kuwatetea mapema Dec 10 na 11 huku dhamana zao
zikiendelea.
Katika shauri hilo la matumizi mabaya ya ofisi linawakabili David
mattaka aliyekuwa mkurugenzi wa ATCL, kaimu ofisa mkuu wa kitengo cha
fedha wa ATCL na Elsaph Ikomba na mkaguzi mkuu wa hesabu za ndani wiliam
haji.
Chanzo-ITV
No comments:
Post a Comment