Tuesday, 3 November 2015

APOSTLE T.B.JOSHUA AKUTANA NA RAIS KIKWETE.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam Jana jioni .

 Mhubiri maarufu duniani TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua jijini Dar es salaam jana jioni tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli .
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha.
TB Joshua amempongeza Rais Kikwete pia kwa kumpata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

No comments: