Sunday, 1 November 2015

Atimaye Israel yaweka Balozi Kamili Tanzania.

Mh,Rais J.M.Kikwete akipokea Hati ya Utambulisho toka kwa Balozi wa Israel nchini BwYahel Vilan.

Atimaye Israel yaleta Balozi Kamili Tanzania Sielewi kwa nini hii imefanyika kimya kimya kwa Kikwete kupokea hati za utambulisho juzi. Kama sikosei hii ni toka tuvunje uhusiano wa kibalozi baada ya vita ya 1967.

Labda baraka za Mungu zitaturudia sasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatano Oktoba 28, 2015; amepokea Hati za Utambulisho za mabalozi wanne ambazo wataziwakilisha nchi zao katika Tanzania.

Katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amepokea Hati za Utambulisho za Mheshimiwa Balozi Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wa Misri, Mheshimiwa Balozi Yahel Vilan wa Israel, Mheshimiwa Balozi Bayani V. Mangibin wa Philippines na Mheshimiwa Balozi Tan Puay Hiang wa Singapore.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

29 Oktoba, 2015

No comments: