![]() |
Diamond Platnumz. |
Akizungumza ofisini kwake Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Diamond alisema katika maisha kila mmoja ana ndoto zake, hivyo ni jambo jema kwamba amefanikisha, lakini hata hivyo, akasema hatua aliyofikia yeye siyo ya kufanya mashindano na mtu, badala yake ni kuchapa kazi kusaka mafanikio zaidi ya maisha yake.
“Kiukweli kabisa nampongeza Wema kwa kununua gari maana hiyo ndiyo ilikuwa mipango ya maisha yake, maneno anayosema kwamba mimi nilimnunulia gari la elfu thelathini ndipo nilipomuona wa ajabu. Sikuona umuhimu wa kunizungumzia pale.
“Hayo ndiyo mambo ya Kiswahili. Mimi siyo mtu wa kushindana kununua gari tena, maana hatua hiyo tayari nimeshapita, zaidi nawaza kupiga kazi na kujitengenezea maisha yangu mapya yatakayoweza kuifanya familia yangu iishi kwa raha na amani kipindi chote cha uhai wangu, najua kuna watu bado wanafikiria mimi ni limbukeni wa vitu kama zamani, kwa sasa sifikirii mashindano, ninaangalia kazi zinazoweza kuniingizia kipato tu,” alisema Diamond.
![]() |
Gari mpya yake Wema Sepetu. |
![]() |
Wema Sepetu akikiss na mpenzi wake wa sasa raia wa Namibia siku ya Sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. |
No comments:
Post a Comment