Friday, 27 November 2015

HABARI SAHIHI KUHUSU KIJANA SHOGA ALIYEOLEWA MAJUZI ULAYA.


Kwa takriban wiki sasa mitandao ya kijamii,blog na vyombo vya habari za udaku zimekuwa zikipeperusha hewani habari inayowajulisha watanzania kuwa kuna mtanzania mwenzao wa jinsia ya kiume,mwenyeji wa Arusha, ameolewa na mzungu huko Uingereza.
Chanzo kilichoanzisha minon`gono hiyo bado hakijawekwa wazi hadi leo ila mimi katika pekua pekua yangu nimekutana na chanzo kimoja cha habari nchini Uganda kinachobainisha kuwa huyo SI`mtanzania` kwa hakika ni Mganda aitwae Jimmy Sserwadda na kuwa ameolewa kwa mara ya pili na mwanaume mwengine raia wa Sweden .
Chanzo hicho cha habari kinasema kuwa awali Sserwadda alikuwa amefunga ndoa na Mganda mwenzie aitwae Lawrence Kaala nchini Sweden katika ndoa inayosemekana kuwa ni ya kwanza kufungwa kisheria kwa raia wa Uganda.Wawili hao walikimbia Uganda wakati wa mchakato wa sheria ya kuharamisha ushoga nchini humo na kisha kufunga ndoa nchini Sweden Jimmy alielezea kisa cha kukimbilia Sweden kwa kusema kuwa Uganda ni sehemu hatari zaidi dnnianii kwa mashoga kuishi.
Alisema yeye na Lawrence walikuwa na uhusiano wa muda mrefu na kwamba siku moja mwaka 2008 alikamatwa na kupigwa sana kwa kitendo chake cha kutetea ushoga na,alipoachiwa aliamua kukimbia Uganda bila ya kumtaarifu Lawrence.Alisema alimficha Lawrence mpango wake wa kutoroka kwa kuwa alijua lazima Lawrence angeng`ang`ania waende wote jambo ambalo linge hatarisha uhai wao. Jimmy alipewa hadhi ya mkimbizi nchini Sweden kwa kigezo kuwa maisha yake nchini Uganda yalikuwa hatarini kwa sababu ya ushoga wake.
Muda mfupi baadae Jimmy alianza shughuli za kikazi katika taasisi ya kutetea haki za mashoga na wasagaji nchini SwedenNa alilenga kuwasaidia wakimbizi waliokuwa na matatizo kama yake. Baadaye Lawrence kwa bahati tu naye alijikuta nchini Sweden alipatwa na mshangao kuona picha kubwa ya Jimmy kwenye jarida moja maarufu nchini humo.
Kaala alifanya mipango ya mawasiliano na Jimmy na hatima yake Kaala alifanikiwa kumpigia simu Jimmy ambaye alipatwa na mshituko kusikia sauti ya jamaa ambae aliamini hatomuona tena maishani mwake na muda si mrefu walikutana ana kwa ana.
Hapo ndipo walipopanga kufunga ndoa kwa ridhaa ya sheria za Sweden. walifunga ndoa siku ya kumbukumbu ya mauaji ya David Kato aliyekuwa maarufu katika harakati za kutetea haki za mashoga nchini Uganda nchini Uganda.
Sherehe ya ndoa iliyofanyika kanisani katika kitongoji cha Jarfalla kilichopo kaskazini mwa mji mkuu wa Sweden Stockholm na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 100 akiwemo Waziri wa Sweden anaehusika na masuala ya Jumuia ya Ulaya mama Brigitta Ohlsson.
Hata hivyo ndoa ya mashoga hao ilidumu miaka miwili tu na kuvunjika na ndipo Jimmy alipoamua kuolewa na mzungu raia wa nchi hiyo.


LENGO LA POST HII NI KUKANUSHA URAIA WA SHOGA HUYU KUWA SI MTANZANIA

No comments: