![]() |
Hashim Rungwe. |
Hashim Rungwe amepiga stori na mtangazaji wa kipindi cha PB,cha Clouds FM,Phillip Mwihava kuhusiana na habari hizo za kutaka kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars.
‘’Unajua Watu wamenipendekeza mimi sijaamua wameamua kunitoa kwenye mitandao ili nipewe timu ya Taifa lakini kwa upande wangu sio jambo baya watu wananitakia jambo jema na pia wananchi wana maamuzi kama nipatapa mwaliko wa kuwa kocha wa Taifa Stars,’’alisema Hashim Rungwe.
Kuhusu mwenendo wa Taifa Stars kwa sasa alisema kuwa yanayotarajiwa na mashabiki siyo yanayotokea.
‘’Kama nitapata mwaliko rasmi na unajua wengi wanafundisha mpira bila kusomea,vijana hawana morali na wengi hawajui kama soka ni maisha,na maisha yao ni ya hali ya chini, mpira ni mali,ni pesa ni faida pia wachezaji hawafaidiki na mpira wanaucheza kuliko wenzao wanavyocheza nchi za nje kwa kifupi wachezaji wetu wana njaa,’’alimalizia Hashim Rungwe.
No comments:
Post a Comment