Mahakama ya ardhi na nyumba mkoa wa Arusha imeamuru mzee wa miaka
themanini Juma Isangu aliyeondoshwa kwa nguvu katika nyumba yake arudi
kwenye nyumba yake na arudishiwe vyombo vyake wakati ikisubiriwa kuanza
kusikilizwa kwa shitaka la msingi huku Bi Jane Fosbroke na wakala wa
mahaka majembe Auction Malt wakitakiwa kulipa ghalama za usumbufu kwa
mzee Juma Isangu.
Akitoa amri hiyo mwenyekiti wa mahakama ya ardhi na nyumba mkoa wa
Arusha Cyriacus Kamugisha amesema kutokana naombi liliowakilishwa na
upande wa mashitaka mahakama imeyapitia kujirishisha na kufanya uamuzi
huo kwa kuzingatia misingi ya kisheria.
Wakizungumza baada ya kutoka kwa amri hiyo mawakili wa wanao mtetea
mzee Juma Isango Willifredy Milambo na Loam Ojale wamesema wamezidhika
na uamuzi wa mahakama kwakuwa awali mteja wao hakutendewa haki kwa
kuondoshwa kwa nguvu katika nyumba yake huku akiwa na nyalaka zilizo
halali huku Bi Janeth akieleza kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama.
Kwa upande wao watetezi wa haki za wazee wamesema ikiwa mahakama
zitafanyakazi kwa uadilifu na kuharakisha maauzi kama ilivyo fanya kwa
mzee huyo zitarudisha imani kwa wananchi huku wakiipongeza mahakama hiyo
kutenda haki kwa mzee Isangu na majira wa mzee huyo ambayo wamehifadhi
familia yake baada ya kunyanganywa nyumba wametoa shukurani kwa uamuzi
uliyo tolewa na mahakama ikiwa ni pamoja na kumpatia wakala wa mahakama
atakaye rudisha vyombo vya mzee Isangu.
No comments:
Post a Comment