![]() |
| Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa |
Stars imetupwa nje ya mashindano kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya mchezo wa awali timu hizo kutoka sare ya kufungana kwa magoli 2-2 kwenye mchezo uliochezwa November 14 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Algeria dhidi ya Taifa Stars (Tanzania) kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa hayuko katika hali nzuri ya kuzungumza na waandishi wa habari na kuomba kuzungumza nao leo kwenye uwanja wa ndege wa Algiers kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Ni kawaida kwa makocha na manahodha wa timu kuzungumza mara baada ya mchezo kumalizika na kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari ambayo huulizwa kuhusiana na mchezo husika.

No comments:
Post a Comment