 |
| Mbwana Samatta akivalishwa taji na mdogowake muda mfupi baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo
asubuhi |
Familia ya Mzee Ally Samatta leo ilikuwepo uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kumpokea na kumpongeza
mtoto wao Mbwana Samatta kwa mafanio makubwa aliyoyapata kwenye soka kwa
kutwaa ubingwa wa Afrika pamoja na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo
kwa mwaka huu.
 |
| Mbwana Samatta (kulia) akilakiwa na babayake mzazi mzee Ally Samatta |
Mzee Ally Samatta ambaye alikuwa ameambatana na familia nzima wakiwemo
kaka na wadogo zake Mbwana Samatta amesema, hawajawahi kwenda kumpokea
Samatta uwanja wa ndege wakiwa kama familia lakini leo waliamua kufanya
kitu cha tofauti kwasababu wanahisi hakuna kitu kingine ambacho wanaweza
kukifanya kikamfurahisha zaidi ya kwenda uwanja wa ndege kama familia
na kumlaki mtoto wao.
 |
| Samatta (katikati) akiwa pamoja na familia nzima iliyokwenda uwanja wa ndege kumpokea |
Mara baada ya kutua uwanja wa ndege, Samatta alijikuta akishindwa
kujizuia kuonsesha furaha aliyokuwanayo baada ya kukutana na familia
yake nzima ikiwa inamsubiri uwanjani hapo kwa ajili ya kumpongeza kwa
mafanikio yake pamoja na kusalimiana nae.
Mashabiki na wadau wa soka nao wakaungana na familia hiyo kumpongeza
Samatta ambaye alikuwa ameambata na Thomas Ulimwengu kabla ya
kuchukuliwa na viongozi wa TFF na kupelekwa sehemu maalumu ambako
watapumzika wakisubiri kuingia kambini kuungana na kikosi kizima cha
Stars.
No comments:
Post a Comment