Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limelazimika kupiga mabomu ya machozi
katika hospitali ya rufaa Bugando ili kumuokoa askari mwenzao aliyekuwa
ameingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, baada
ya mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
(Chadema ) mkoa wa Geita Alphonce Mawazo kuwasili kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi wa kidaktari.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 11.30 jioni baada ya viongozi wa
Chadema na wafuasi wao kufikisha mwili wa mawazo ambaye katika uchaguzi
mkuu wa mwaka huu aligombea ubunge wa jimbo la Busanda, huku askari hao
waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi wakimkamata mwenyekiti
wa baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi kwa mahojiano zaidi.
Mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema amezungumzia
kifo cha Alphonce Mawazo, aliyewahi kuwa diwani wa kata ya Sombetini
Arusha kwa tiketi ya chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2010.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita Alphonce Mawazo aliuawa kinyama
baada ya kushambuliwa kwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana
baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Geita.
No comments:
Post a Comment