Monday, 16 November 2015

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Dr. Tulia, amteua kuwa mbunge.


Dr Tulia Ackson,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo asubuhi ametengua uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu Dr Tulia Ackson, Mwansasu na kumteua kuwa Mbunge.

=========================

Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene, ameithibitisha kutenguliwa na kuteuliwa kwa Dk. Tulia.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila, amekiri kupokea taarifa ya uteuzi wa Dk. Tulia mapema leo asubuhi.

Awali kabla ya uteuzi huo, Dr Tulia alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo pia hapo jana Novemba 15, 2015 alikuwa ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.

 

No comments: