![]() |
| Akiwa mikononi mwa polisi. |
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amewasilisha waraka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akitaka kushikiliwa na kuzuiwa kwa mali zote za mtuhumiwa wa madawa ya kulevya ‘unga, Muharami Abdallah au maarufu kwa jina la ‘Chonji’ na mkewe, Mwalibora Nyanguri kuhamisha umiliki, kupangisha au kuombea mikopo.
![]() |
| Vitendea kazi alivyokutwa navyo. |
Maombi hayo dhidi ya Chonji na mkewe yaliwasilishwa kwa hati ya
dharura mahakamani hapo Septemba 13, mwaka huu mbele ya Jaji Wilfred
Dyansobela.
MBALI YA CHONJI NA MKEWE
AG ameiomba mahakama hiyo imzuie Chonji, mawakala wake au mtu mwingine yeyote kwa niaba yake, kuhamisha umiliki wa mali, kupangisha nyumba au kuombea mikopo (ili serikali ifuatilie uhalali wa upatikanaji wake.
![]() |
| Mjengo anaomiliki. |



No comments:
Post a Comment