Baada ya kuachia kwa kishindo video ya Baki na Mimi, msanii wa muziki Mr
Blue amesema kuwa, huo ndio mwanzo wa kufunguka na kuwekeza pesa kwa
upande wa muziki wake, hii ikiwa ni kazi yake ya kwanza kuingia mfukoni
na kuigharamia kikubwa.
Mr
Blue amesema kuwa, kwa muda mrefu sana amekuwa akifanya video za kuunga
unga na washkaji, bila kuhusisha gharama zozote kutoka mfukoni kwake,
akieleza kuwa Baki na Mimi ndiyo video iliyomsumbua kukamilisha visa
vyote alivyoviimba, sehemu ya gharama ikiwa ni kukodisha limousine yenye
gharama ya shilingi milioni 1 kwa siku, gauni la zaidi ya shilingi laki
4 na vitu vingine vingi ambavyo amevilipia mpaka kazi nzima ili
kuwasilisha kazi nzuri kwa mashabiki.
Blue amesema kuwa, kazi hii inavunja utaratibu wake wa awali wa kuendesha sanaa yake kwa ubahili kidogo, akiwa amejipanga sasa kwaajili ya kuwekeza pesa ili kupata pesa kutoka katika muziki.
Iangalie VIDEO hapo chini.....

No comments:
Post a Comment