Monday, 14 December 2015

Vyama vya kijamii 1,268 vyafutiwa usajili.

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefuta vyama vya Kijamii 1,268 baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yao kisheria.

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefuta vyama vya Kijamii 1,268 kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na sheria zilizowekwa katika uendeshaji wa vyama pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NG’0s).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga amesema kuwa kufutwa kwa vyama hivyo ni kutokana na kukiuka masharti ya uwendeshaji wa taasisi ikiwemo kutolipa ada kwa mujibu wa sheria.
Katika ufutwaji wa vyama hivyo chama kimojawapo kilichofutwa ni chama cha wapiga picha nchini ambacho kimeshindwa kukidhi vigezo vya uendeshaji na kushindwa hata kuendesha vikao vyake.
Nantanga amesema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutwa na baada siku 21 kuanzia leo, kama havitatoa kusudio la kujitetea basi navyo vitafutwa.
Amesema kufuatana na kanuni ya vyama inayoundwa na kifungu cha 38 cha sheria ya vyama vyote vya kijamii vinapaswa kulipa ada ya kila mwaka.

No comments: