Tuesday, 8 December 2015

Polisi watahadharisha Ongezeko la bei za nauli Krismasi na Mwaka Mpya.

Jeshi la Polisi lakataza wamiliki wa mabasi kupandisha nauli kipindi hichi cha sikukuu, atakayekiuka agizo, kufikishwa mahakamani.

-Baadhi ya kampuni za usafirishaji kila mwisho wa mwaka zimekuwa zikipandisha nauli kutokana na wananchi wengi kwenda katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.




JESHI la Polisi nchini, Kikosi cha Usalama Barabarani, limesema mmiliki wa kampuni ya gari la abiria litakalojaribu kuongeza nauli ya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi katika kipindi cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, atakamatwa na kufikishwa Mahakamani .
Upandishaji nauli kinyume cha nauli elekezi ambayo hutolewa na Serikali umekuwa ukifanywa na baadhi ya kampuni za usafirishaji kila mwisho wa mwaka kutokana na wananchi wengi kwenda katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya mapunziko na vile vile kusherekea sikukuu ya Krismasi na mwisho wa mwaka.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kampuni au mtu atakayeongeza nauli ya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya atakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Aidha, amebainisha kwamba kutokana na kasumba ya watu au kampuni kuwatoza nauli abiria tofauti na ilivyopangwa na mamlaka husika, wamejipanga kupambana na kundi hilo la watu na kuwa yeyote atakayepatikana hawatapigwa faini bali watafikishwa mahakamani moja kwa moja.
Abiria kuuziwa tiketi feki
Katika hatua nyingine, abiria kadhaa Jijini Dar es Salaam wametahadharisha Jeshi la Polisi pamoja na SUMATRA kuongeza kasi ya kufanya ukaguzi wa tiketi wanazouziwa na mawakala ili wasikwame kwenda makwao kutokana na ongezeko la mawakala bandia katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo wanaouza tiketi feki.
Abiria wakiwa katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoni na nchi jirani cha Ubungo Jijini Dar es salaam

No comments: