Friday, 29 January 2016

Linex: ‘Mzungu’ ndiye mwanamke pekee niliyemkuta na ‘Bikira’ maishani mwangu.

Mwanamuziki wa Bongo flava, Sunday ‘linex’ Mjeda, ameweka wazi kuwa tangu apate akili na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, Ex wake ambaye ni mzungu kutoka Finland ndie msichana pekee aliyemkuta katunza usichana wake.
Akizungumza kupitia kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm mapema leo asubuhi, Linex amedai kuwa hata kuachana kwao hakukuwa kwa ugomvi bali ni kutofautiana mahitaji.
“Unajua nchi za ukanda ule wa Scandnavia wanawake wanajitunza sana, na mzungu ndiye mwanamke pekee maishani mwangu niliyemkuta na ‘Bikira'” alisema.
Hit maker huyo wa Kwahela, amesema mara ya mwisho kuwasiliana na binti huyo wa Kizungu ni baada ya kuonekana picha za ‘ndoa’ feki  kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyomfanya binti huyo kuamini kuwa Linex ameoa.

No comments: