Tuesday, 12 January 2016

SERIKALI YA MAGUFULI YAPANGA KUYAFUNGIA MAGAZETI HAYA KWA KOSA HILI

Rais Dkt,John magufuli.

Gazeti la Jambo leo na Raia Tanzania yote kwa pamoja ambayo yanatoka kwa siku, yako mbioni kufungiwa na Serikali ya Rais John magufuli.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Ofisi ya msajili wa Magazeti nchini,ambazo mtandao huu umezipata zinasema kwa sasa ofisi hiyo ya msajili itafikia uamuzi baada ya kubainika Magazeti hayo yamekiuka sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Makosa ambayo yanadaiwa kufanywa na magazeti hayo ni ile ya wamiliki wa magazeti hayo kuyauza kinyemela bila ya hata kuishirikisha ofisi ya msajili wa magazeti nchini kama sheria ya magazeti inavyotaka,pia kuchangia kuikosesha serikali mapato kutokana na uuzwaji huo .
Taarifa za magazeti hayo kuuzwa zilipotiwa wiki mbili zilizopita kuwa,Gazeti la Jambo leo ambalo mwanzo lilimilikiwa na Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania ambapo kwa sasa inadaiwa kuwa kampuni hiyo imeliuza Gazeti hilo kwa Kampuni ya Quality Media Group ambayo inamilikiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya mpira ya Yanga,Yusuf Manji.
Mbali na hilo,Gazeti la Raia Tanzania pia nalo limeuzwa pia kutoka kwa Bodi ya wanahisa wa Gazeti la Raia Mwema ambapo kwa sasa Bodi hiyo imeliuza Gazeti hilo kwa Kampuni ya TSN Super Market, inadaiwa sababu ya Bodi ya wamiliki wa Raia Tanzania kuliiuza gazeti hilo baada ya kuporomoka kimauzo. “Ninachokwambia magazeti haya lazima yafungiwe ndugu,maana yamekiuka sheria ya magazeti ambayo inawataka walete taarifa ofisi ya msajili,lakini hawa hajafanya hivyo ,tena wameikosesha mapato serikali maana wanauziana magazeti kinyemela huku serikali haipati mapato,nakuhakikishia lazima yafungiwe tu.”kimesema chanzo chetu kilichopo ndani ya ofisi ya msajili wa Magazeti.

No comments: