WAZANZIBARI leo wamesherehekea miaka 52 ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka
1964, ambayo yaling’oa utawala wa Sultani kutoka Oman na kuwezesha
wazalendo wengi kushika hatamu ya kuongoza nchi.
Katika kilele cha sherehe hizi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amehutubia taifa katika uwanja wa Amaan.
Matukio mengine makubwa yaliyofanyika katika uwanja huu ni Rais Shein kukagua gwaride la heshima la vikosi ya ulinzi na usalama, vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Amepokea maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Unguja.
Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na Viongozi wastaafu, Mzee Mwinyi, Benjamin Mkapa Aman Karume na Wengine Wengi wa Kitaifa, walishiriki sherehe hizi zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani katika sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Z'bar.
Vilevile Mkuu wa Majeshi Brigedia Aden Mwamnyange amehudhuria. Viongozi wengi wa Kitaifa wamehudhuria pia.
Maalim Seif Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amekwepa Sherehe hizi.
Hizi sherehe za mapinduzi leo zimepoa. Hii inadhiirisha tatizo kubwa la mkwamo wa kisiasa lilipo Zanzibar, Si kama miaka ya nyuma.
=========
Shein: Kwa upande wa Zanzibar, kama sote tunavyofahamu, tume ya uchaguzi ilifuta uchaguzi wa Zanzibar tarehe 28 October mwaka jana baada ya kubainika kutokea kasoro kadhaa kama zilivyoelezwa na tume ya uchaguzi ya Zanzibar. Kadhalika uamuzi huo wa tume ulitangazwa katika gazeti rasmi la serikali tarehe 6 November mwaka 2015 kwamba tume ya uchaguzi ya Zanzibar imeyafuta matokeo yote ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na kwamba uamuzi wa tume kutangaza tarehe nyingine ya kurudia uchaguzi mkuu wa Zanzibar utatangazwa baadae.
Nawaomba wananchi waendelee kuishi kwa amani na waendelee kupendana huku tukisubiri tume ya uchaguzi ya Zanzibar itangaze tarehe nyingine ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar. Kwa hio uchaguzi kwa mujibu wa katiba na sheria ya Zanzibar ya uchaguzi utarudiwa.
HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. DK. ALI MOHAMED SHEIN, KATIKA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 52 YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR, AMAAN STADIUM
TAREHE 12 JANUARI, 2016
Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan;
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa;
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad;
Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar,
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi;
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar,
Mheshimiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi;
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa,

Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete;

Mheshimiwa Dk. Salmin Amour Juma;
Rais Mstaafu wa Zanzibar,
Mheshimiwa Dk. Amani Abeid Karume;
Rais Mstaafu wa Zanzibar,
Waheshimiwa Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Mheshimiwa Job Ndugai;
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho;
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,
Mheshimiwa Othman Chande Mohamed;
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Omar Othman Makungu;
Jaji Mkuu wa Zanzibar,
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa,
Mheshimiwa Abdalla Mwinyi Khamis;
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,
Viongozi mbali mbali wa Serikali na Vyama vya Siasa,
Ndugu Wananchi,
Mabibi na Mabwana,
Assalamu Aleikum,
Awali ya yote, napenda nianze kwa kumshukuru Mola wetu Mtukufu mwenye kustahiki kushukuriwa na viumbe vyote kwa kutujaalia uhai na afya njema tukaweza kukutana katika hadhara hii muhimu kwa historia na harakati za maendeleo ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa jumla. Leo tarehe 12 Januari, 2016 tunaadhimisha kilele cha sherehe za miaka 52 tangu yalipofanyika na kufanikiwa kwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964.
Mwenyezi Mungu awape malazi mema waasisi na viongozi wetu wa Mapinduzi waliokwishatutangulia mbele ya haki na walio hai, Mwenyezi Mungu awape afya njema na umri mrefu ili tuzidi kunufaika na hekima zao. Mwenyezi Mungu aijaaliye nchi yetu amani, umoja, mshikamano zaidi na atupe mafanikio katika utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo na kutuongezea ustawi wa jamii yetu.
Ndugu Wananchi,
Kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar, napenda nimpongeze kwa dhati Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan; Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiongoza Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuchaguliwa kwenu, ni kielelezo cha imani waliyonayo wananchi kwenu na kwa Chama cha Mapinduzi. Natoa shukurani zangu za dhati kwenu, kwa kuja kuungana nasi katika sherehe hizi za maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Tunakukaribisheni kwa furaha kubwa pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mliohudhuria.
Kadhalika, napenda nitoe shukurani zangu za dhati kwa mabalozi, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, taasisi mbali mbali, wananchi na wageni waalikwa wote kwa kuhudhuria kwa wingi katika sherehe hizi muhimu na adhimu ambazo zimefana sana. Kuwepo kwetu hapa siku hii ya kilele na mahudhurio makubwa kunadhihirisha kwamba Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 yanathaminiwa sana na yataendelea kudumishwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ndugu Wananchi,
Leo ni siku adhimu na muhimu kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla ambapo miaka 52 iliyopita waliikata minyororo ya utawala wa kikoloni na kisultani ambao ulidumu kwa miaka 132. Wananchi wanyonge walioongozwa na Chama cha Afro Shirazi walijitolea muhanga kufanya Mapinduzi dhidi ya wakoloni, mabwanyenye na mabepari waliokuwa wakiendeleza vitendo vya udhalilishaji, dhulma, unyonyaji na ubaguzi kwa wananchi.
Madhila waliyotendewa wananchi yalihusu masuala yote muhimu ya maisha yakiwemo kubaguliwa katika elimu, matibabu, makaazi na matumizi ya ardhi na ubaguzi wa kukoseshwa haki za kiraia katika nchi yao wenyewe. Haya yote leo yanabaki kuwa ni historia baada ya Waasisi wa Mapinduzi wakiongozwa na Jemedari wake Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Chama cha ASP kufanya Mapinduzi tarehe 12 Januari, 1964. Huo ndio mwanzo wa utawala wa wanyonge wa Zanzibar na kupata uhuru wao wa kweli, unaozingatia misingi ya usawa, utu na kuturejeshea heshima ya wafanyakazi na wakulima nchini mwetu iliyopotea kwa kutawaliwa.
Leo tunaposherehekea miaka 52 ya Mapinduzi, vile vile, tunasherehekea umoja wetu unaotokana na nchi mbili zilizokuwa huru, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu umetokana na dhamira ya dhati ya vyama vyetu vya ukombozi vya ASP na TANU na sasa CCM pamoja na uongozi bora na thabiti wa Waasisi wa nchi yetu, hayati Mwalim Julius Kambarage Nyerere na hayati Mzee Abeid Amani Karume.
Ndugu Wananchi,
Kwa hakika tuna wajibu wa kuwashukuru na kuwaombea dua Waasisi wa Mapinduzi kwani wao ndio msingi wa mafanikio makubwa wa maendeleo tuliyoyapata. Katika kipindi chote cha miaka 52, wananchi wote kwa nyakati tafauti wamefaidika na matunda ya Mapinduzi kutokana na malengo yake na mipango ya maendeleo iliyowekwa.
Kwa hivyo, maadhimisho ya sherehe hizi yanatukumbusha umuhimu wa kuendelea kuyaheshimu, kuyatetea, kuyalinda na kuyadumisha Mapinduzi yetu, kwa faida ya kila mmoja wetu. Katika kuyathamini na kuyaenzi Mapinduzi yetu, Serikali imeamua kujenga mnara maalum wa kumbukumbu ya Mapinduzi katika eneo la Michenzani, Mwembekisonge, uliozinduliwa mwaka jana. Naomba wananchi mwende mkautembelee mnara wa aina yake huu pale mtakapopata nafasi ambapo pia mtapata nafasi ya kuelezwa historia ya Mapinduzi iliyotayarishwa katika vyumba maalum.
Ndugu Wananchi,
Jitihada za Serikali, wananchi na washirika wetu wa maendeleo zimetuwezesha kuitekeleza mipango mikuu ya maendeleo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya 2020, MKUZA Awamu ya Pili na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2010-2015 tuliyoitekeleza kwa kiwango kinachokadiriwa kufikia asilimia 90 pamoja na Malengo ya Milenia. Maelezo nitakayoyatoa yanadhihirisha mafanikio yaliyopatikana katika mwaka 2015.
Ndugu Wananchi,
Katika mwaka 2015, Tume ya Mipango ya Zanzibar imeratibu mapitio ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUZA II) unaomaliza muda wake mwezi wa Juni 2016. Rasimu ya mwanzo ya mkakati mpya imefikia hatua ya kuchangiwa maoni na wahusika mbali mbali na inategemewa kuanza kutumika rasmi kuanzia bajeti ya mwaka 2016 /2017.
Vile vile, Serikali imefuta Sheria namba 1 ya mwaka 1999 ya miradi ya maridhiano na kutunga Sheria mpya ya mashirikiano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) namba 8 ya mwaka 2015. Ni matumaini ya Serikali kwamba wawekezaji binafsi wataitumia fursa ya mashirikiano baina ya sekta hizo mbili, kupitia sheria mpya, kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi.
Ndugu Wananchi,
Kutokana na umuhimu wa utafiti, Serikali kupitia Tume ya Mipango kwa kushirikiana na COSTECH inatayarisha Mpango wa Utafiti wa Zanzibar wenye kushirikisha sekta zote. Rasimu ya awali ya mwongozo wa utekelezaji wa tafiti imetolewa ili kazi ya utafiti ifanyike kitaalamu kwa lengo la kupata taarifa sahihi na kuondoa kero za wananchi.
Katika mwaka 2014, Serikali iliandaa programu maalum za utekelezaji wa Matokeo kwa Ustawi kwa kupitia mfumo wa maabara katika sekta ya Utalii, uimarishaji wa biashara na upatikanaji wa Rasilimali Fedha. Utekelezaji wa programu hizi umeonesha mafanikio ya kutia moyo. Kwa
sasa, Tume iko katika hatua za matayarisho ya maabara ya Elimu na Afya kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika. Maabara hizo zinatarajiwa kufanyika mwaka huu.
Ndugu Wananchi,
Licha ya kuendelea kuwepo kwa matukio mbali mbali yanayoathiri kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia, uchumi wetu umeendelea kuimarika katika kila mwaka. Mwaka 2014 Pato halisi la Taifa lilikua na kufikia asilimia 7.0. Hali hii imechangiwa zaidi na kuimarika kwa sekta ya viwanda na sekta ya huduma kwa kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaoingia nchini kutokana na kuwepo kwa vivutio vya utalii na amani na utulivu. Kadhalika, Pato la Mtu binafsi limeongezeka hadi kufikia TZS 1,552,000 (USD 939) mwaka 2014 ikilinganishwa na TZS 1,384,000 (USD 866) mwaka 2013 sawa na ongezeko la asilimia 12.1. Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015, pato la mtu binafsi lilitakiwa lifikie TZS 884,000 ifikapo mwaka 2015. Ni dhahiri kwamba pato la mtu binafsi limepindukia kiwango kilichokadiriwa.
Ndugu Wananchi,
Katika kipindi cha robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2015, kasi ya ukuaji wa uchumi imefikia asilimia 6.1 na katika robo ya pili ya mwaka 2015 imefikia asilimia 7.0. Kuendelea kuimarika kwa hali ya uchumi kwa robo mwaka ya kwanza na ya pili kwa mwaka 2015 kumetokana na kuimarika kwa sekta ya viwanda, sekta ndogo ya malazi, huduma za chakula, huduma za fedha, ufugaji, bima pamoja na ukuaji wa sekta ndogo ya ujenzi.
Katika mwaka 2015, kasi ya mfumko wa bei za bidhaa na huduma nchini imeendelea kuwa ya tarakimu moja kutoka asilimia 5.6 mwaka 2014 kufikia asilimia 5.7 mwaka 2015. Serikali inaendelea na juhudi za kudhibiti kasi ya mfumko wa bei nchini kwa kupunguza ushuru wa bidhaa muhimu zinazoingizwa nchini na kuwasaidia wakulima kwa kuwapatia pembejeo kwa beif nafuu ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
Ndugu Wananchi,
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeongeza ufanisi katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kudhibiti uvujaji wa mapato hayo. Katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka wa fedha 2015/2016, mapato ya ndani yalifikia TZS Bilioni 188.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka 2014/2015 ambapo TZS Bilioni 172.5 zilikusanywa, sawa na ongezeko la mapato la asilimia 9.2. Vile vile, Serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha mapato ikiwemo kupunguza misamaha ya kodi katika baadhi ya miradi ya uwekezaji na kufanya marekebisho ya viwango vya ada mbali mbali. Kadhalika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha kodi mpya ya miundombinu, ili kuhakikisha tunakuwa na fedha za kuiendeleza na kuitunza miundombinu yetu.
Ndugu Wananchi,
Serikali iliendelea kuwashajiisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika sekta zote kuu za kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2015, jumla ya miradi 31 yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 316.0 imeidhinishwa katika sekta mbali mbali katika miradi hio, miradi mingi ni ya utalii. Miradi hii itakapomalizika itatoa nafasi za ajira 2,500.
Juhudi kubwa zilifanywa zilizopelekea kuanzishwa kwa utekelezaji wa kuyaendeleza Maeneo Huru ya Uchumi kwa vitendo. Mradi wa Ujenzi wa Mji Mpya wa Fumba umeanza, ambapo kiwanda kikubwa cha maziwa kimejengwa na kimeanza kazi Julai, 2014. Mji huo utajumuisha ujenzi wa nyumba 650 zitakazouzwa kwa watu mbali mbali. Ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kuanza Februari mwaka huu. Kadhalika, bandari ndogo itakayotoa huduma kwa wananchi na wageni itajengwa katika eneo hilo. Serikali, kwa kushirikiana na Kampuni ya Union Property Developer na Coastal Dredging hivi sasa inaendelea na ujenzi wa miundombinu, ikiwemo barabara mpya zenye upana wa mita 15, mita 30 pamoja na barabara kuu ya mita 60.
Ndugu Wananchi,
Kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa wa kibiashara pamoja na hoteli kubwa za kisasa, nyumba za kuishi, uwanja wa ndege mdogo na uwanja wa kimataifa wa golf wa kisasa vitajengwa. Kampuni ya Pennyroyal ya Gibralter imetenga jumla ya Dola za Kimarekani milioni 800 kwa ajili ya mradi huu. Kampuni hiyo hivi sasa inaendelea na ujenzi barabara ya kisasa inayotoka Mkwajuni kupitia Kijini hadi Mbuyutende na imefikia hatua nzuri.
Katika kuliendeleza eneo la Bwawani mnamo mwezi wa Novemba 2015, Serikali ilitiliana saini Mkataba na Kampuni ya Quality Group Limited ambayo itaanzisha mradi mkubwa wa kuendeleza Hoteli ya Bwawani na maeneo yaliyoizunguka. Kampuni hiyo imetenga Dola za Marekani zipatazo Milioni 200 zitakazotumika kwa ajili ya kuifanyia matengenezo makubwa Hoteli ya Bwawani, ili ifikie kiwango cha nyota tano. Kadhalika, kampuni
hiyo ya Quality Group Limited itajenga majengo ya biashara na kituo cha mikutano ya Kimataifa katika eneo hilo la Bwawani.
Aidha, Serikali imeidhinisha mradi wa uimarishaji wa Hoteli ya Mtoni Marine , wenye lengo la kutengeneza ufukwe maalum kwa ajili ya mapumziko ya wageni na wenyeji. Sambamba na uimarishaji huo, utaanzishwa mji mdogo wa kisiwa kwa lengo la kuikuza sekta ya utalii.
Ndugu Wananchi,
Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) nao umeshajiika kuwekeza katika ujenzi wa majengo ya kisasa, ili kubadilisha taswira ya Zanzibar. Katika mwaka huu wa fedha, 2015/2016, ZSSF imeanza kutekeleza Mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo la Mbweni Unguja. Mradi huu unajumuisha ujenzi wa jumla ya majengo 18 ya ghorofa 7 kila moja na yatakapomalizika, jumla ya nyumba (flats) 252 zitapatikana. Mradi huu unatarajiwa kumalizika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Ndugu Wananchi,
Katika mwaka 2015, suala la kuimarisha mazingira ya biashara lilipewa umuhimu mkubwa. Serikali ilichukua hatua ya kuhakikisha kuwa bidhaa za chakula zinakuwepo nchini wakati wote. Takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 hakukuwa na upungufu wa bidhaa hizo. Serikali imeanzisha Baraza la Kusimamia Utoaji wa Leseni kwa lengo la kuweka mfumo mzuri na ulio bora katika utoaji wa leseni na vibali vya biashara.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ililinunua jumla ya tani 2,826.5 za karafuu 2,826.5 zenye thamani ya TZS bilioni 39.5 kutoka kwa wakulima katika mwaka 2014/2015, hadi kufikia tarehe 4 Januari, 2016, Serikali ilinunua jumla ya tani 3,235.1 zenye thamani ya TZS bilioni 45.3.
Kwa upande wa mauzo, katika mwaka 2014/2015, Serikali iliuza nchi za nje jumla ya tani 2,766.2 za karafuu zenye thamani ya TZS bilioni 53.3. Kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2015, Serikali imeuza karafuu nchi za nje tani 2,122.0 zenye thamani ya TZS bilioni 36.0. Msimu wa karafuu wa mwaka huu bado unaendelea na wakulima wanaendelea kuuza karafuu zao ZSTC na matarajio ya Serikali ni kununua tani 5,500 za karafuu.
Kadhalika, katika kipindi cha mwaka 2014/2015, Serikali imetoa mikopo yenye thamani ya TZS milioni 342.3 kwa wakulima 126 wa karafuu wa Unguja na Pemba. Mikopo hiyo imewasaidia kununua pembejeo na vitendea kazi. Nachukua nafasi hii kuwapongeza wakulima wa Unguja na Pemba kwa juhudi zao wanazozichukua katika kuliendeleza zao la karafuu kwa kushirikiana na Serikali.
Aidha kwa lengo la kuliendeleza zao la karafuu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilizindua Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu Zanzibar ambao Shirika la ZSTC limeweza kulipa fidia kwa walioanguka kwenye mikarafuu jumla ya TZS milioni 60 na kutoa mikopo.

No comments:
Post a Comment