Wimbo wa Zigo “remix” ulioimbwa na Ay akimshirikisha Diamond Platnumz imepigwa marufuku kupigwa katika vituo vya televisheni.
Akizungumza kwa mshangao mkubwa, Ay amesema alipokea barua yenye amri hiyo kutoka kwa rafiki yake ambae anafanya kazi katika chombo kimoja cha habari. AY alisema barua hiyo ilitoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ikisema kwamba video hiyo inakiuka maadili.
” Sijaelewa maadili gani kwa sababu kama maadili niliyokosea mimi ni kushoot kwenye swimming pool : na kama kwenye swimmig pool watu nimevalisha jeans au maturubai , hapo nitakuwa nimekosa maadili. ”
Kwa masikitiko, AY aliongeza “Mavazi ya kwenye swimming pool yako kila mahali, hata kwenye Taarifa za Habari (Michezo) wanaonyesha waogeleaji : kama hiyo pia ni kukiuka maadili ni sawa.
Inashangaza mamlaka zetu wanafocus kwenye kufungia nyimbo zetu na kuacha video za nje. Sijawahi sikia muziki wa Kenya, Uganda au Marekani umefungiwa. Kama wanaona nyimbo za Nicki Minaj zina maadili halafu Zigo ya Ay haina maadili baasi unaacha tu iwe hivyo ”

No comments:
Post a Comment