Wednesday, 17 February 2016

Rais Magufuli alikabidhi Jeshi la Polisi jukumu la ulinzi Bandarini!

Rais John Magufuli, alitaka Jeshi la Polisi kurejesha kitengo cha ulinzi bandarini

-Pia wametakiwa kulinda eneo la mita za mafuta kama ilivyokuwa awali.


Leo hii Mh Rais ameagiza Jeshi la Polisi kushika jukumu la ulinzi kwenye bandari hii ni katika jitihada za kudhibiti wizi bandarini!

Mtakumbuka jukumu la ulinzi hapo nyuma lilikuwa chini ya jeshi la polisi lakini wakapewa TPA na sasa Rais ameamua kuwa jeshi la polisi liwe na jukumu ya kulinda bandari na mali zake!

Pia kule kwenye mafuta na Flow meter pia jeshi la polisi limekabidhiwa jukumu la ulinzi!

Tuzidi kumuombea Rais wetu mpendwa maana ni wazi ni chaguo la Mungu!

Chanzo: EATV HABARI 

No comments: