Tuesday, 5 April 2016

BABU YAKE WASTARA AFUNGUKA SABABU YA MJUKUU WAKE KUSHINDWANA NA MBUNGE.

Babu wa muigizaji wa kike ‘Grade one’ Bongo, Wastara, amefunguka moja kati ya sababu zilizofanya kuvunjika Ndoa kati ya mjukuu wake huyo na Mbunge wa Donge kupitia CCM Sadifa Khamis Juma.
Akizungumza na Times Fm, Babu huyo amesema kuwa Sadifa alikithiri kuwa na utovu wa nidhamu kiasi hata cha kumzushia yeye anavunja ‘amri ya sita’ na Mjukuu wake.
Mbali na kumzushia hayo, Babu huyo aliweka bayana kuwa Mbunge huyo mwenye cheo ndani ya umoja wa vijana CCM, alifikia hatua ya kuwatongoza wafanyakazi wa ndani ili awe nao kimapenzi.
Aidha ameweka bayana kuwa, kwa sheria za Dini ya Kiislamu Ndoa hiyo siyo halali mara baada ya Mbunge huyo kutamka hadharani kwamba amemuacha Wastara.
“Wastara hataki kurudiana na Sadifa, kutokana na vitendo alivyokuwa akivifanya, imefikia wakati mpaka wale wafanyakazi wa ndani wananambia babu, babu, baba huku anatutongoza njoo uone na meseji tunazo kwenye simu.
“alafu hana adabu anafikia hatua ya kuniambia mimi nalala na mtoto wangu Wastara, aisee sijui atakuja kunieleza vipi kwa hilo” Alisema.

No comments: