Saturday, 9 April 2016

Dkt Shein atangaza baraza lake la mawaziri.

Akitangaza baraza hilo mchana wa leo katika ikulu ya Zanzibar, Dkt Shein amesema hatua hiyo ni kwa mujibu wa katiba, na amezingatia mpango wa serikali yake kuwaletea wazanzibari maendeleo kwa haraka.
Baadhi ya vigezo alivyotumia ni uadilifu pamoja na kubana matumizi na kusema kuwa utaratibu wa kidemokrasia umekamilika kwa mujibu wa katiba.
Katika baraza hilo, Dkt Shein amepunguza idadi ya wizara kutoka 16 zilizokuwepo katika kipindi cha kwanza cha awamu yake hadi 13 katika awamu hii ya pili.
Amesema kikosi alichokiteua kitamsaidia kwa ukamilifu kutimiza lengo lake la kuendesha serikali kwa uwazi na ukweli huku akiwataka vyombo vya habari kutenda haki na kutoegemea upande mmoja na kuandika mabaya peke yake badala yake kuandika mazuri pia yanayofanywa na serikali.
Amewataja mawaziri hao na wizara zao kama ifuatavyo:-
Issa Haji Ussi – Waziri Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Haruna Ali Suleiman – Waziri wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
Abdi Omary Kheri – Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI na Idara Maalum
Mohamed Abood Mohamed – Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Dkt Khalid Salim Mohamed – Waziri wa Fedha na Mipango
Mahamoud Thabit Kombo – Waziri wa Afya
Riziki Pembe JUma – Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Balozi Amina Salum Ali – Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko
Balozi Ali Abeid Karume – Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Rashid Ally Juma – Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
Hamad Rashid Mohamed – Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Nurdin Kastiko – Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto
Salama Abood – Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira
Pia amewataja manaibu waziri 7 kuwa ni:
Harusi Said Suleiman - Wizara ya Afya
Mmanga mjengo Mjawili – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Mahamed Ahmed Salum – Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Lulu Mshamu Khamis – Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Chum Kombo Khamis – Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
Juma Makungu Juma – Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira
Khamis Juma Maalim - Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
Dkt Shein pia amewajumuisha Juma Ally Khatib na Said Sud Said kutoka vyama vya upinzani kuwa wajumbe katika baraza hilo.

No comments: