Jana mchana through social media taarifa za msanii wa Bongo
Fleva,Tundaman kupata ajali zilisambaa ambapo Tunda Man alifanikiwa
kutoka salama kwenye ajili hiyo mbaya iliyotokea Eneo la Idetelo,
katikati ya Nyololo na Makambako, mkoani Iringa na kusababisha kifo cha
dereva aliekua akiendesha gari hilo alietambulika kwa jina moja la Aron.
Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man yalidai kuwa “Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki”.

No comments:
Post a Comment