Msanii wa Bongo Fleva, Cyril Kamikaze aliyedaiwa kumgonga trafiki. Msanii wa Bongo Fleva, Cyril Kamikaze yamemkuta baada ya kuswekwa nyuma ya nondo za mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar, kufuatia msala wa kudaiwa kumgonga na kumburuza kwa gari trafiki aliyemsimamisha barabarani, aliyejitambulisha kwa jina la Afande Francis. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ambacho ni mmoja wa mashuhuda, tukio hilo lililokuwa kama sinema ya kivita lilijiri wiki iliyopita majira ya saa 5:00 asubuhi jirani na Hospitali ya Magomeni, Dar, wakati trafiki huyo akitekeleza majukumu yake ya kuongoza magari barabarani. Ilidaiwa kuwa, trafiki huyo alimsimamisha Cyril ambaye alimpuuza na kumgonga. “Alichokifanya Cyril ni unyama, kama alijijua ana makosa angesimama tu na kumsikiliza.
“Kwanza alimgonga, yule trafiki akajihami kwa kurukia juu ya gari kwa mbele (kwenye boneti), akazidi kukimbiza gari ili ammwage barabarani. “Hata hivyo, mashuhuda walimsifu sana yule trafiki maana kama asingekuwa yupo fiti kwa kujiokoa, basi angekufa,” kilisema chanzo hicho. Kwa upande wake trafiki huyo alipoombwa na Ijumaa Wikienda kuelezea mkasa huo, huku akiwa na masikitiko makubwa alisema, hadi sasa haamini kama yupo hai kutokana na ujasiri mkubwa alioutumia kujiokoa, kwa kuwa kila anapojiuliza Cyril alikusudia nini, anakosa jibu. “Niliona gari ndogo lenye ‘tinted’ nzito linakuja, nikaamua kulisimamisha, cha ajabu likasimama lakini baada ya kuona nakaribia kulifikia akaliondoa kwa kasi na kunigonga. Ndipo nikachukua bodaboda kulikimbiza hadi kwenye Kona ya Kwa-Shehe Yahya.





No comments:
Post a Comment