Mwaka
2012-2013 Serikali ya Tanzania ilikopa Dola za kimarekani milioni 600
‘trilioni 1.3’ kutoka benki ya Standard ya Uingereza kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya Maendeleo kwa makubaliano ya kulipa deni hilo pamoja na
riba ya 1.4% inasemekana katika mazingira yasiyojulikana fedha
iliongezwa na kuwa 2.4%.
Kwa
taarifa ya Serikali iliyotolewa na aliyekuwa katibu Mkuu Ombeni Sefue
siku kadhaa zilizopita alieleza kuwa katika mkopo huo hawakuhitaji
wakala lakini mwaka 2013 iligundulika kuwa fedha Taslimu Dola milioni 6
ziliingizwa katika akaunti ya kampuni ya Egma ambayo mwenyekiti wake ni aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ Harry Kitilya.
April 01 2016 Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania, Shose Sinare wamefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam kwa tuhuma
mbalimbali zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja na kosa la
kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Wakili wa Serikali upande wa Mashitaka Oswald Tibabyekomya ametoa maelezo kuwa……>>>’kosa
ambalo linawagusa pamoja ni kughushi nyaraka ambao ni mkataba wa
makubaliano unaoonesha kwamba Stanibic Bank iliingia makubaliano na
kampuni ya Egma kwa ajili ya kutafuta mkopo kwa ajili ya Serikali,
mkataba ambao ulikuwa wa uongo, kiasi cha fedha kilichohusika kwenye kosa la kujipatia fedha kwa udanganyifu ni dola za kimarekani milioni 6′
Kutokana na makosa yanayowakabili, watuhumiwa wamenyimwa dhamani na kesi yao itasomwa tena April 8 2016.






No comments:
Post a Comment