Raia
wawili wa China wamehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela au kulipa faini
ya Sh milioni 50 kila mmoja, kwa kosa la kusafirisha Sh milioni 20
kwenda nchini China bila kibali kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT).Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha baada ya washtakiwa
kukiri kosa. Washtakiwa waliohukumiwa kifungo hicho ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Feng Shi Trading, Sun Ning (39) na Fen Quan
(51).Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema washitakiwa wamepatikana
na hati ya makosa matatu, na kwa kosa la kwanza kila mmoja atalipa faini
ya Sh milioni 10 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela, kosa la
pili faini ya Sh milioni 20 au jela miaka mitano, kosa la tatu faini ya
Sh milioni 20 au jela mwaka mmoja.
Alisema kwa makosa yote, adhabu yao ni sawa na kifungo cha miaka 11 jela au kila mmoja kulipa faini ya Sh milioni 50, lakini adhabu ya kifungo inakwenda sambamba hivyo ni sawa na kifungo cha miaka mitano jela.

No comments:
Post a Comment