Kondakta
Hamimu Seif (42), mkazi wa Mwananyamala Ujiji, jijini Dar es Salaam,
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka
kumtishia kumuua kwa maneno Rais Dk. John Magufuli (pichani), kwa
kujitoa mhanga.Mshtakiwa huyo alisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao, alidai kuwa
Machi 10, mwaka huu, katika baa ya Soweto iliyopo Kijitonyama Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alimtishia kumuua Rais Dk.
Magufuli.Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitamka: "Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Dk. Magufuli, nipo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumwangamiza," alikaririwa akisema mshtakiwa huyo.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana shitaka hilo na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.Hakimu Riwa alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. milioni mbili kila mmoja.

No comments:
Post a Comment