 |
| Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape
Nnauye (kushoto) samabamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul
Makonda wakiwa msibani hapo. |
 |
| Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Ndanda Kosovo, King Dodoo akiweka mambo sawa msibani. |
 |
| King Blaise wa FM Academia akiimba kwa huzuni. |
 |
| Mama yake Ndanda Anne Mariane Kombe akilia kwa uchungu |
 |
| Mke wa pili wa marehenu, Infrancie. |
 |
| Francie akilia mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe. |
 |
| Totoo Zebingwa akimsalimia Waziri wa Michezo na Sanaa Bw,Nape Nnauye. |
WAZIRI wa Habari, Vijana, Sanaa,
Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mh. Paul Makonda wamewaongoza mamia ya waombolezaji katika
shughuli ya mazishi ya staa wa Muziki aliyefariki mwishoni mwa wiki
iliyopita, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ katika Makaburi ya Kinondoni jijini
Dar,
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya
Mazishi ya mwanamuziki huyo, King Dodoo marehemu anatarajiwa kuzikwa leo
Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi
yamefanyika kwenye nyumba ya Ubalozi wa Congo DRC iliyopo
Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo alisema wameamua kumzika marehemu
hapa nchini kufuatia wosia wake alioutoa mbele ya Waziri wa Habari,
Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza na
wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika kikao hicho Ndanda alisimama na
kusema endapo akifa basi maiti yake izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo
mahali alipopatia mafanikio makubwa ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu
ambayo atazikwa na watu wengi kuliko Lubumbashi alikozaliwa.
No comments:
Post a Comment