Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) ,Augustine Mrema,amedai Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad,alistahili awe amekwamatwa kwa kutoa Kauli za uchochezi. Mrema ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu ashindwe kiti cha Ubunge jimbo la Vunjo,Mkoani Kilimanjaro katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka jana,alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya hali ya amani visiwani Zanzibar.
Kauli ya Mrema imekuja huku Jeshi la polisi Zanzibar,likitarajia kumhoji Maalim Seif wakati wowote.
Alidai kuwa kitendo cha Maalim Seif kujitangazia matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana ni kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment