Thursday, 9 June 2016

JACKLINE WOLPER NA NISHA WATOANA MAPOVU KISA'HARMONIZE'


Bongo movies bado kunazaliwa Drama kila kukicha, na sasa ni Kisanga kati ya waigizaji wawili wa kike Jcqueline Wolper na Salma ‘Nisha’ Jabu ambao wamerundumuana mitandaoni kisa msanii wa WCB Harmonize.
Mtiti ulianza baada ya Nisha kupost picha inayowaonesha Ben Pol, Raymond, Nuh Mziwanda na Rich Mavoko na kuipa Caption ya, ” Mmoja kati ya hawa amejaa kwenye galary ya simu yangu na moyoni mwangu,otea A B C AU D? enhe. he sa hv siweki hadharani maana nna phd ya kunyakuliwa, sa hivi ni kumpost kwa mwendo kasiii yaani wengi wengi simtaji ng’ooo.” Baada ya post hiyo ikaibuka Comment ya Wolper ikimtaka Nisha aweke wazi mwandani wake aliyewahi nyakuliwa, ndipo Nisha akaamua kuandika waraka kama unavyosomeka hapo chini,
“Ok guys kuna picture niliweka saa 4 asbh leo,za wasanii kadhaa wa music ambao niliweka na caption yangu kwa furaha zangu tu,” aliandika Nisha kwenye post nyingine.
“Ila baada ya lisaa limoja ikaja coment hiyo ya msanii mwenzangu sikudhungumza chchte,i was like ok nikacheka tu. Then zikaja comments nyingi za kumuuliza kulikoni kuandika hivyo. Masaa mawili yaliyopita ukaandikwa waraka mzito mrefu unaosema. “Nisha aandaa show Mtwara ya kumnasa Harmonize ila Wolper akagundua hilo akaamua kuongozana naye Harmo hadi huko kukwepa hilo (NA MANENO MENGI YA ZIADA YA UONGO.”
 “Ikimbukwe show imeshapita km week na haya maneno yamezuka leo baada ya hiyo comment.
Guyz tuje kwenye point
KWANZA KABISA SIJAMLENGA YYTE KWA NILIYEANDIKA NILIANDIKA KWA MAPENZI YNG KM NILIVYOANDIKA JANA STATUS YA VIDONDA VYA TUMBO,TENA HADI WADOGO ZNG NIKAWAAMBIA TAZAMA NACHEZA NA AKILI ZA WATU. NIMESHANGAA HABARI ZA UONGO KUSAMBAZWA ZIDI YANGU TENA BAADA YA COMENT HII KWANGU,” aliongeza. “POINT YA PILI KWA YYTE ANAYEULIZA NIMEANZA LINI UPROMOTA guyz mimi ni mfanyabiashara na kwenye pesa nipo,show ya MTWARA imenigharimu si chini ya ml.18 unadhani naweza poteza pesa zote hizo kisa mapenzi?sina ujinga huo wa akili. 
NA SIJAWAHI KUMTAKA NA SITOTARAJI KWANZA SIJAZOEA KUPITA ANAPOPITA MTU HASWA NNAYEMJUA.”
“TATU nimeandaa show ingine ramadhan ya 13 DAR-ES-SALAAM inahusu ramadhan, nna SHOW SKUKUU YA IDD MOSS NA IDD PILI MIKOANI ZOTE MM NDO MUANDAAJI NA KUNA WASANII WAKUBWA TU JE HAO PIA NATAKA KUWANASA? HE. IFIKE HATUA TUSIWE TUNABALANCE MTU MMOJA NA PIA SIO KILA ASIYEDHUNGUMZA NI MNYONGE SANA ILA KUNA WKT DRAMA HAZINA MUDA INABIDI UPIGE KAZI MAANA MAISHA YANAENDA MBELE HAYARUDI NYUMA. NB:SHUKRAN KWA WEWE UNAYESAMBAZA UJUMBE HUU WA UONGO SINA CHA KUKWAMBIA NIMEPITIA MENGI MAKUBWA SO HILI KM NACHEZA MDAKO. (mwenye uelewa kaelewa chanzo cha story inayosambaa imetoka wapi,nimeandika hapa kwa manufaa ya mashabiki zangu wote watakaobahatika kusoma habari hizo za uongo.

No comments: