Leo February 8, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
ameingia kwenye awamu anayoiita ni ya pili kwa kutaja orodha ya watu
ambao watahitajika kufika Polisi Central Dar es salaam kusaidia taarifa
na maelezo kwenye mapambano ya kutokomeza dawa za kulevya Dsm.
Kwenye
orodha hiyo iliyosambaa mitandaoni kwenye jina namba 54 kuliandikwa
Philemoni Mbowe na hivyo habari zikaanza kusambaa kwamba sio Freeman
Mbowe aliyetajwa.
Jioni hii
Paul Makonda amewaambiwa Waandishi wa habari kwamba jina la kwanza
kwenye namba 54 lilikosewa na inatakiwa kuandikwa Freeman Mbowe hivyo
anaehitajika Ijumaa ni Mheshimiwa Freeman Mbowe.




No comments:
Post a Comment