Thursday, 5 April 2018

ALIYEMUUA MKEWE KWA KISU NCHINI UINGEREZA APANDISHWA RASMI KIZIMBANI.


Mtanzania Kema Salum (38), leo amefikishwa Mahakamani at Crown Court Hearing kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma Kisu mke wake Marehemu Leyla (36), mbele ya mtoto wake wa kiume Terry mwemye umri wa Miaka (12) katika nyumba ya Marehemu Leyla Mtaa wa Kirkstall Avenue/Heringey, London...

Mbele ya Judge Anuja Dhir mtuhumiwa amesomewa Mashitaka huku akitafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na Mkalimani wa Mahakama...hata hivyo kutokana na mgomo wa Wanasheria wa bure wanaoajiriwa na Serikali ya Uingereza Mtuhumiwa amekosa Public Advocate na Judge Dhir aliamuru kesi hiyo kutajwa tena Tarehe 20/June/2018 kwa ajili ya Dhamana na kesi kuanza kusikilizwa Tarehe 24/September/2018 ...

Judge ameamuru Mtuhumiwa kurudishwa Rumande mpaka Tarehe 20/June kama ataruhusiwa kupewa Dhamana...kutokana na Mtuhumiwa kuwa hana uwezo wa kujilipia Mwanasheria wa Kujitegemea itabidi asubiri mpaka Wanasheria wa Bure wa Serikali watakapomaliza mgomo..

No comments: