MSANII WA FILAMU TANZANIA MAHSEN AWADH a.k.a DR CHENI MWISHONI MWA WIKI HII ALIPATWA NA MKASA WA KULISHWA SUMU,AKIWA KATIKA SHEREHE YA HARUSI AMBAPO YEYE AKIWA KAMA MSHEREHESHAJI KATIKA SHUGHULI HIYO,DR CHENI ALIKULA CHAKULA ALICHOPAKULIWA NA MMOJA WA WAHUDUMU KATIKA SHEREHE HIYO,AMBAPO ANADAI BAADA YA KULA CHAKULA HICHO HALI YAKE ILIBADILIKA GHAFLA NA KUANZA KUISHIWA NGUVU,NDIPO ALIPOTOKA NJE YA UKUMBI ILIPOKUWA IKIFANYIKA SHUGHULI HIYO ILI AWEZE KUPATA HEWA ZAIDI LAKINI HALI YAKE ILIZIDI KUWA MBAYA HADI KUFIKIA KUKIMBIZWA HOSPITALINI HARAKA KWA MATIBABU ZAIDI,KWA HIVI SASA HALI YA DR CHENI INAENDELEA VIZURI,KWA TUKIO HILO MSANII LULU MICHAEL AMEONYESHA KUHUZUNISHWA SANA NA KITENDO HICHO,IKIZINGATIWA KUWA MSANII HUYO ALIKUWA MSTARI WA MBELE WAKATI WA KUPIGANIA KUPATIKANA KWA DHAMANA YA KESI YAKE YA MAUAJI DHIDI YA MSANII MWENZIE "THE GREAT STEVEN KANUMBA"TUNAMTAKIA HERI DR CHENI AFYA YAKE IZIDI KUIMARIKA,AENDELEE KUTUBURUDISHA/KUTUFUNZA NA FILAMU ZAKE NZURI.
No comments:
Post a Comment