Friday, 16 August 2013

CHIDI BEENZ AFUNGUKA JUU YA KUTUMIA KWAKE MADAWA YA KULEVYA.

RAPPER MAHIRI NCHINI TANZANIA,RASHID MAKWILO,A.K.A CHIDI BEENZ AMEFUNGUKA JUU YA YEYE BINAFSI KUWA MTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA KWA MUDA MREFU,JAMBO LILILOMFANYA KUSHUKA KATIKA UFANISI WA KAZI YAKE YA MUZIKI,CHIDI BEENZ,AMBAYE WAPENZI WAKE WAMETOKEA KUMPACHIKA MAJINA MENGI{A.K.A}KAMA MFALME WA ILALA,CHUMA NA KING KONG,AMEFUNGUKA HAYO JUZI KWENYE KIPINDI CHA XXL CHA CLOUDS FM,ALIPOKWENDA REDIONI HAPO KUITAMBULISHA SINGLE YAKE MPYA "NAKAZA ROHO",AKIFAFANUA JUU YA HILO CHIDI AMEONGEZA KUWA ILIKUWA NI VIGUMU KWA FANS WAKE NA WATU WENGINE KUJUA KAMA YEYE ALIKUWA NI MTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA KWA JINSI ALIVYOKUWA AKIJIWEKA,HASA KATIKA HALI YA USAFI,UKIANZIA MWILI,MAVAZI NA HATA CHAKULA BORA ALICHOKUWA AKIZINGATIA,JAPO ALICHOKIONA NI MAPUNGUFU KWAKE NI JINSI ALIVYOKUWA AKIJIONA BINAFSI KATIKA MUONEKANO WAKE WA NDANI YAANI KUWA MTU ALIYEJAA CHUKI NA MINOMA KILA ANAPOKUWA MBELE YA JAMII,AKIONGEZA JUHUDI ALIZOFANYA ILI KUACHANA NA UTUMIAJI HUO WA MADAWA YA KULEVYA,NI BAADA YA KUHUDHURIA CLINIC MAALUM NCHINI KENYA INAYOSAIDIA SANA WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA,WENYE NIA YA KUJITOA KATIKA UTUMIAJI WA MADAWA HAYO,"NILIMWAMBIA MAMA LAZIMA NIENDE NIKATIBIWE"CHIDI ALISISITIZA JINSI ALIVYOKUWA AKIMSHIRIKISHA MAMA YAKE JAMBO HILI,KWA HIVI SASA CHIDI ANAELEZEA KUWA HALI YAKE NI SAFI KIAFYA,NA UWEZO WA KULA UMERUDI ZAIDI YA KIPINDI ALIPOKUWA AKITUMIA MADAWA HAYO,UWEZO WA KUFANYA MAZOEZI NA KUFIKIRI VYEMA.

No comments: