Tuesday, 27 August 2013

MWAKYEMBE AENDELEZA TIFU "AIRPORT"{D.S.M}WALIOTIMULIWA WOTE WAKABIDHIWA BARUA,NAKUTAKIWA WASIKANYAGE AIRPORT KABISA.

KATIKA HALI ILIYOZUNGUMZIWA NA WENGI KUWA NI VITA ILIYOPATA AMIRI JESHI KAMILI,HII NI BAADA YA KUKABIDHIWA RASMI BARUA ZAO ZA  KUSIMAMISHWA KAZI MAOFISA USALAMA WANNE,AMBAO WANAHUSISHWA MOJA KWA MOJA NA TUKIO LA KUSAFIRISHA KILO 180 ZA UNGA{MADAWA YA KULEVYA}WALIOKAMATWA NAO AGNES MASOGANGE NA MDOGO WAKE NCHINI AFRICA YA KUSINI.
KAULI HIYO YA KUKABIDHIWA BARUA MAOFISA HAO WA USALAMA UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM ILITOLEWA RASMI JANA NA KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI TANZANIA BW,RAMADHAN MALETA KWA NIABA YA WAZIRI MWAKYEMBE,WALIOPATIWA BARUA ZAO NI YUSUPH ISSA,JACKSON MANYONYI,JULIANA THADEI NA MOHAMED KALUNGWANA,AKISISITIZA KAULI YA MH,WAZIRI WA UCHUKUZI BW,HARRISON MWAKYEMBE,MAOFISA HAO HAWATAHITAJIKA KUKANYAGA KABISA KWENYE MAENEO YA VIUNGA VYA UWANJA WA NDEGE KWA KIPINDI HIKI AMBAPO SHITAKA LAO LIPO MAHAKAMANI KWA AJILI YA KUTOLEWA MAHAMUZI..KATIKA HALI YA KUONYESHA KUONGEZA NGUVU JUU YA MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA,ULINZI UMEIMARISHWA ZAIDI KIWANJANI HAPO,IKIWEMO MITAMBO MIPYA ILIYOFUNGWA UWANJANI HAPO NA MBWA WAUKAGUZI AMBAO WATAENDELEA KUWEPO UWANJANI HAPO.

No comments: