Friday, 27 September 2013

PATA KUMFAHAMU SAMANTHA LEWTHWAITE"THE WHITE WIDOW".

YAFUATAYO NI BAADHI YA MAMBO AMBAYO WENGI WALIKUWA HAWAYAJUI TOKA KWA MSHUKIWA WA TUKIO LA KIGAIDI "WESTGATE"-KENYA,SAMANTHA LEWTHWAITE"THE WHITE WIDOW"KAMA ANAVYOJIITA,
1-ANA UMRI WA MIAKA 29,AMEZALIWA JIJINI BUCKINGHAMSHIRE,NI MWANAMKE ANAYEZUNGUMZIWA NA KUNDI LA EL SHABAAB,KUWA NI MWANAMKE MWENYE AKILI SANA,SAMANTHA NI MJANE WA MWENYE WATOTO WAWILI ALIYEWATELEKEZA WATOTO WAKE TOKA 2007 BAADA YA KUHAMIA NCHINI KENYA AKIJIUNGA NA EL SHABAAB

2-TAHARIFA ZA KIPOLISI ZINADAI KUWA SAMANTHA NDIYE MKUFUNZI WA MAMBO YA KIJIHAD KWA WANAWAKE WALIOCHINI YA KUNDI LA EL SHABAAB,PIA SAMANTHA NI NDIYE ALIYEKUWA MKE WA GERMAINE LINDSAY GAIDI ALIYEJIUA KWENYE TUKIO LA KIGAIDI KWA KUJILIPUA YEYE NA WOTE WALIOKUWEMO KWENYE TRENI YA CHINI YA ARDHI NCHINI UINGEREZA JULAI 5th 2013.
3-KWA MUJIBU WA NYARAKA TOKA KWA SAMANTHA ZILIZORIPOTIWA NA GAZETI LA DAILY MAIL LA UINGEREZA,ZINADAI KUWA WHITE WIDOW ANAWALEA WATOTO WAKE ILI WAJE KUWA WANAHARAKATI WENYE IMANI KALI,MUME WAKE WA PILI BW,HABIB SALEH GHANI NAYE INASEMEKANA ALIUWAWA KWENYE TUKIO LA KIGAIDI.
4-MWANAMKE ANAYETAMANI KUONA WATOTO WAKE WANAKUJA KURITHI KAZI YAKE YA KUJITOA MUHANGA JUU YA UJAHIDINA.

5-NI MTAALAMU WA KUTENGEZA VIFAA VYA KUFICHA SURA,PUA NA KICHWA,UKIACHANA NA TAALUMA YAKE YA UBUNIFU WA MAVAZI YA KIISLAM,KAZI ALIYOIANZA AKIWA CHINI YA UANGALIZI WA EL SHABAAB NCHINI KENYA.
6-INDAIWA KUWA NDIYE MUHUSIKA WA TUKIO LA KIGAIDI NCHINI UGANDA,TUKIO LA JUNI 24th NCHINI UGANDA,WAKATI WA MASHINDANO YA EURO 2012,KWENYE MECHI KATI YA ENGLAND VS ITALY,AMBAPO GURUNETI LILILORUSHWA KWENYE BAA WALIPOKUSANYIKA WAPENZI WA SOKA,SHAMBULIO LILILOUWA MTU MMOJA, TUKIO LILILOSHUHUDIWA NA MTOTO ISACK SIMIYU{23}ALIYEKUWA NJE YA JENGO LA BAA YA JERICHO ILIYOLIPULWA,MTOTO HUYO BAADA YA KUHOJIWA VIZURI NA POLISI NA KUKIRI KUMUONA ALIYELIPUWA BOMU HILO KUWA NI MWANAMKE WA KIZUNGU ALIYEFICHA SURA YAKE KWA KITAMBAA,NDIPO POLISI WALIPOMLETEA PICHA NNE TOFAUTI ZA WANAWAKE,ALIICHAGUA YA SAMANTHA NA KUTHIBITISHA KUWA NDIYE MUHUSIKA.

7-NI GAIDI WA KIKE ANAYETISHA ZAIDI,HII NI BAADA YA KUONDOKA ULRIKE MEINHOF MWANZILISHI WA KUNDI LA RED ARMY,AMBALO LILIHUSIKA NA MILIPUKO YA MABOMU UJERUMANI MAGHARIBI MIAKA YA 1970.
8-ALIPOKIMBIA KWENYE NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI MJINI MOMBASA-KENYA,KILIKUTWA KIJITABU KILICHOANDIKWA KUWA ANATAKA WATOTO WAKE WAJE KUWA NI WATU WAKUJITOA MUHANGA,HUKU ZIKIKUTWA BUNDUKI ZA KISASA,RISASI NA MAPIPA YA KEMIKALI,YANAYOTUMIWA NA MAGAIDI KUJILIPULIA PINDI WANAZIDIWA NGUVU.
9-JINA LAKE LA KIISLAM NI ASMAA SHAHIDAH BINT ANDREWS,WAKATI MTOTO WAKE WA KIUME ANAITWA ABDUL RAHIM FAHEEM JAMAL,ALIYEZALIWA STOKE MANDEVILLE{2009},KATIKA CHETI CHAKUZALIWA CHA MTOTO WAKE HAKUNA JINA LINALOTAMBULISHA JINA LA BABA MZAZI WA MTOTO HUYO,SAMANTHA ALISILIM AKIWA NA UMRI WA MIAKA 18,AKIACHANA NA UVAAJI WA MAVAZI YA KIFASHENI ZA KIDUNIA NA KUHAMIA KWENYE MAVAZI YA KIISLAM IKIWEMO HIJAB. 
10-ALISOMA MASOMO YA DINI NA SIASA KWENYE SHULE IITWAYO ORIENTAL & AFRICAN STUDIES HUKO RUSSEL SQUARE LONDON UMBALI WA MTUPO WA JIWE TOKA PALE ALIPOJIUWA MUMEWE KWA KUJILIPUA.

No comments: