MADEREVA wote wa daladala Manispaa ya
Morogoro leo wamegoma kutoa huduma ya usafiri wakilalamikia kukamatwa
hovyo na maafande wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika manispaa hiyo.
Akizungumza na tovuti hii, mmoja wa
madereva wa daladala hizo, Bw. Ramadhani Shukuru alisema kwamba kwa siku
gari linakamatwa mara mbili na kwamba ukifikishwa kituoni unalipishwa
faini ya shilingi 90,000/=
"Unakamatwa asubuhi unalipa 90,000/= makosa matatu, ukiachiwa na
kuanza kazi ukifika Kihonda unakamatwa tena ukijitetea askari
anakwambiaa yeye hausiki na kukamatwa kwako kwani amekukamata kwa makosa
mengine unaenda tena kituoni wanakukamua 90,000/= nyingine kesho
unakamatwa tena, sasa si bora tuegeshe magari tukalime matombo!" alisema
Rama.
 |
KUTOKANA NA MGOMO HUO,WANAFUNZI IMEBIDI KUTUMIA USAFIRI WA MALORI KUWAHI SHULENI. |
|
|
|
 |
Wanafunzi wa shule mbalimbali za Manispaa ya Morogoro wakiwa kwenye lori baada ya mgomo wa madereva daladala leo. |
 |
Wanafunzi
wa shule mbalimbali za Manispaa ya Morogoro wakisubiri usafiri wa
kwenda shule bila mafanikio katika kituo cha mabasi kilichopo Mkoani
Morogoro. |
No comments:
Post a Comment