Wednesday, 19 March 2014

PICHA-KAMPENI ZA CCM KUELEKEA UBUNGE{CHALINZE} ZAZIDI KUSHIKA KASI

 Msafara wa Mgombea Ubunge katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Kikwete ukielekea kwenye Mkutano wa Kampeni katika Kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Mchinga,Mh. Said Mtanda (kulia) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze Machi 18,2014,wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (wa pili kushoto walioketi).

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze Machi 18,2014.Katika Mikutano yake kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo hilo,Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo.



Wananchi wa Kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze wakimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akilakiwa na wanakijiji wa Kijiji cha Msigi Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akisikiliza kwa Makini hotuba ya Mwenyekiti wa Kijiji hicho,Mzee Juma Mwinyigoha (hayupo pichani).

Ukafika wakati wa Chakula cha Mchana na wakaingia kwenye kibanda ya Mama ntilie ndani ya Kijiji cha Msigi na kuanza kupata msosi.

Mgombea akitoka kwa Mama Ntilie baada ya kupata msosi.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Msigi,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze



Wazee wakifurahi jambo wakati wa Hotuba ya Mgombea wao.

Meneja wa Kampeni za CCM Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi

Moja ya Changamoto ambazo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Kikwete amesema atakabiliana nazo pindi atakapopata ridhaa ya kuwa kiongozi wa wana Chalinze ni kusimia ukarabati wa Barabara katika vijiji mbali mbali ndani ya Jimbo hilo,moja wapo ikiwa ni hii inayotoka Msigi mpaka Kisanga.

Burudani ya Ngoma za Asili.


MwanaCCM akifatilia Mkutano kwa umakini.




No comments: