Tuesday, 11 March 2014

HATIMAYE MAUJANJA SAPLAYAZ WAZIKA TOFAUTI ZAO NA CLOUDS FM.

Baada ya malumbano ya miaka mingi sasa rappers wanaofahamika kwa jina la ‘Maujanja Saplayaz’ wamezika tofauti zao chini na mkurugenzi wa vipindi na utayarishaji Clouds Media Group Bwana Ruge Mutahaba.

Mapacha waliamua kwenda kumaliza mgogoro wao wenyewe baada ya miaka mingi iliyotokana na movement ya Vinega na Ant Virus kutokana na kugundua ugomvi haukuwa na faida kwao zaidi ya kuvuruga mipango mingine ya kimaendeleo.

Akiongea na kipindi cha ‘Show Time Next Chapter’ cha RFA jana na mmoja wa kundi hili Dotto aka D Wa Maujanja Saplayaz alisema ni wao wenyewe wameamua kufanya hivyo kwa manufaa yao” Kuna vitu vingi vya kluvifanya na si hii tu, idea ilikuwa ni sisi wenyewe twende tukaongee nae kwamba ‘hii beef tunaimaliza’ tunaweka mambo clear kwamba sisi tupo poa hatuna nanini yoyote tuendelee na mambo mengine.” alisema
D akifunguka kuhusu ugomvi umeharibia mambo mengi sana kwa kusema “Kwa upande wetu sisi umetuharibia vitu kwasababu tulikuwa tunafatiliana zile, kwasababu unaweza ukapata show sehemu fulani unashangaa ile show inaingiliana na mambo ya siasa so mnakutwa mnashindwa kwenda kufanya show au mnaenda sehemu kuomba kwa ajili ya kufanya shiow watu wanaogopa hawa jamaa ni nini na nini si unajua zile ni vitu vingi inatuharibia. Halafu kuna wasanii wengi hawataki kufanya kazi na sisi hivyo tunashindwa kuendelea.”

No comments: